Hiba Abu Nada

Mwandishi kutoka Gaza. Alizaliwa mwezi wa sita tarehe ishirini na nne, mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na moja. Kitabu chake cha kwanza, ‘Oksijeni si ya waliokufa’ (Oxygen is not for the Dead) ilichapishwa mwaka wa elfu mbili kumi na saba. 

Tarehe saba Oktoba, Saa kumi na mbili na dakika hamsini na nne asubuhi. 

Tulienda kulala tukifikiria kuhusu mambo kawaida; mtihani wa chuo kikuu, kununua nguo mpya, wasiwasi kuhusu kuomba kazi, alafu ghafla, sauti ya kengele inabadilika. Mitihani imeghairiwa, shule zimefungwa, bunduki zinalia kila mahali, Al-Jazeera inabadilika kuwa nyekundu, tunawasha redio na Telegram, kwa akili tunaaza kuashirisha mipango yetu yote. Kila kitu Gaza kinabadilika papo hapo. 


Tarehe nane Oktoba, saa tano na nusu asubuhi. 

Matangazo yetu yote ni tanzia; si kutoka nyumba ya maiti, mazishi, matangazo ya kifo gazetini, kusorora kurasa ni kama kutembea katika jiji lililokuwa na mazishi kila mahali. Aisee, uzito was siku hizi . . . 


Tarehe nane Oktoba, saa nne na dakika mbili usiku

Amerika wanataka kutuma ndege kusaidia jeshi ya kizayuni. Ni sawa. Inshallah tukipata uhuru tutaifanya iwe mkahawa unaoelea majini. 


Tarehe tisa Oktoba, saa sita na dakika thelathini na nne mchana 

Risasi hizi zinatoka wapi?

Kutoka moyo yetu iliyojaa huzuni ya mgaza. 


Tarehe tisa Oktoba, saa kumi na dakika hamsini na nne jioni

Kwa vita zote zilizopita, ni kama wazayuni walikuwa wamepanga watakao ua. Saa zingine ilikuwa mafamilia, zingine ilikuwa misikiti, au barabara, au sehemu za mipaka, au miji, au fleti. Hatimaye, kulikuwa na mpango wa milipuko tuliotambua, sisi tuliokuwa tunalipuliwa, na kutumia ujuzi huo, tuliweza kujua malengo, njia na urefu wa milipuko. 

Muda huu hakuna mpango. Kila kitu kinalipuliwa na vita zote zimechanganishwa kwa hii. Gaza yote, kutoka kaskazini hadi kusini, inalipuliwa bila mpango, kuna mauaji yasiyosita,kila kitu kinauliwa. Ila, ni uvumilivu wetu na imani yetu inayotuwezesha kuangalia ndege za kivita na kutulia badala ya kulia. Iwapo tutalia baada ya kimya, inatuwezesha kusema, “Eh Mungu, hatuna msaidizi ila Wewe.”


Tarehe tisa Oktoba, saa kumi na mbili na dakika thelathini na tisa jioni

Marafiki wapendwa, 

Tunainiga muda ambapo tutatengwa na dunia ili mji wetu utokomezwe kwa muda mfupi kabisa. Muda ambapo hatutaweza kuwasiliana na yeyote aliye nje au ndani ya mji wetu. Giza haijaingia lakini makombora bado yanangushwa. Hadi muda huo ufike nawasihi mtufunike kwa mafuriko ya maombi na utume ujembe au hata neno ya uthabiti na uhuru kwa binafsi yetu. Tunaacha Gaza na yote iliyomo ndani mwake kwa Mungu, Mchungaji, Aliye na Nguvu. 


Tarehe kumi Oktoba, saa tatu na dakika ishirini na tisa asubuhi

Siku ikianza, baada ya kuhakikisha tuko hai, tunaanza kuhesabiana—nani yuko, nani amezikwa—na si watu tu, hata barabara na nyumba zetu. Mji yote imefanywa shahidi. 


Tarehe kumi Oktoba, saa mbili na dakika hamsini na sita jioni

Nakimbilia Kwako

nikitoroka maumivu na uchungu

ile mistari saba inayorudiwarudiwa

nazirudia

ninakiri

kutoka fosforasi, ladha ya chungwa

na rangi ya mawingu

naKukimbilia

waliopenda na kufariki

vumbi itatawanya 

na watacheka


Tarehe kumi na moja Oktoba, saa tano na dakika tisa asubuhi

Gaza alifanya yote ilikyowezekana kukabiliana na ukandamizaji huu. Aliyoyafanya yalizidi tuliyowaza, akapaa juu ya mipaka ya inayowezekana na isiyowezekana, akapasua makatazo yote, akatambulisha uthabiti utakaofunzwa na wanahistoria, utaopewa jina lake Gaza. Baada ya uongo kufichuliwa, wanasiasa na unafiki wao kuondolewa, na utu dhaifu kujiangukia: Gaza atabaki hadithi isiyowezekana wala kueleweka, atakuwa na rekodi ambayo miji, ustaarabu, na jeshi wataweza kufikia labda wakati wa nabii na miujiza pekee. 

Tumefanya inahostahiliwa kupata haki zetu, kupigana, kuvumilia, kwa binafsi ya nchi yetu na watu wote wanaokandamizwa duniani, hatuna ya kujuta au kutupa huzuni. Mbele ya Mungu na sisi wenyewe, tunahaki inayofaa, wajibu wetu katika agano hii ilikuwa kuvumilia na kujitahidi, yaliyobaki ni ya Mungu tunayeamini na tunayempa imani. Tukifa, itakuwa kitambulisho cha heshima na tukiishi, tutaambia dunia yote hadithi yetu. Miongoni mwa hali hizo, tunazo hizia zetu—machozi, subira, huzuni, ukumbuvu, tumaini na uchungu. 

Iwapo tutakufa, wacha niseme kwa binafsi yetu, kuna watu hapa waliokuwa na ndoto za kusafiri, kupenda, kuishi, na vitu zingine. 

Tupo chini ya ndege, na Mungu yu juu zao, na yu juu yao. 


Tarehe kumi na mbili Oktoba, saa nane na nusu mchana

Familia nzima zinafariki, si mmoja au wawili. Kila mtu kwa familia anakufa na Gaza inageuka kuwa nyika, kaburi kubwa kutoka mlango wa Ligi ya Kiarabu hadi jukwaa la Umoja wa Mataifa (United Nations), na tunatazama kaburi yetu na kimya, uzito na usikivu kwa Mungu. 


Tarehe kumi na tatu Oktoba, saa sita na dakika kumi na tano mchana

Leo ni Ijumaa. Ninaona kama haijakuwa wiki, imekuwa siku moja refu iliyogawika kwa mashahidi na walioumia na kifo nyingi. Hatujui tunayongoja. 

Tarehe kumi na tatu Oktoba, saa mbili na dakika kumi na tatu jioni

Tunaishi kwa dakika hapa, muda uo huo tunapo penda picha mtandaoni, tunapo zima kengele ya kutuamsha, unapoita mtoto wako, unaweza mwita na hakuna jibu. Kifo kina kasi kutuliko. 


Tarehe kumi na tano Oktoba, saa kumi na moja na dakika kumi na tisa jioni

Sauti tunayosikia ni sauti ya kifo inayopita juu yetu kuchagua wengine. Bado tu hai, tunasikia kifo ya wengine na kusema: Asante Mungu, sauti ya mwisho waliosikia haikuwa sauti ya kombora. Wanaosikia sauti ya kombora wanaishi. Tuko hai kwa sasa. 


Tarehe kumi na tano Oktoba, saa mbili na dakika arobaini na saba jioni

Tuko angani, tunajenga mji mpya, madaktari bila wagonjwa au damu, walimu bila madarasa zilizo na msongamano wa wanafunzi, familia mpya bila uchungu na huzuni, waandishi wa habari kupiga picha ya paradiso, washairi kuandika kuhusu upendo usioisha, wote wakiwa watu wa Gaza. Mbinguni, Gaza mpya—isiyokandamizwa wala kuzungukwa—inakuja. 


Tarehe kumi na saba Oktoba, saa tano na dakika arobaini na sita asubuhi

Watoto wanakufa bila kuwahi kuitwa kwa majina yao!

Tarehe kumi na nane Oktoba, saa mbili na dakika hamsini na nane usiku

Picha za familia zetu ni mkoba wa viungo au rundo la majivu au sanda tano za ukubwa tofauti zilizofungwa na kulazwa kando kando. 

Picha za familia zetu ni tofauti na za familia zingine, lakini wako pamoja, waliishi pamoja na wakafariki pamoja. 


Tarehe kumi na nane Oktoba, saa tatu na dakika kumi na saba usiku

Tukifa, mjue tulikuwa thabiti na tayari, na mseme tulikuwa watu wenye dai iliyofaa. 

Tarehe kumi na tisa Oktoba, saa saba na dakika kumi mchana

Marafiki wangu wanapungua, wanafanywa majeneza yaliyotawanyika hapa na pale. Siwezi washika marafiki wangu baada ya makombora kuwatupa hewani, siwezi warudisha hai wala kuwapa rambirambi wala kulia. Sijui nifanyeje. Kila siku wanapungua kidogo kidogo. Hawa si majina tu, ni watu kama sisi, na uso na majina tofauti. 

Eh Mungu, tufanye nini? Eh Mungu, usoni mwa kifo hii isiyoshiba. 

Hakuna yeyote wa kuwarudisha, hata akijinyima. 

Tarehe kumi na tisa Oktoba, saa saba na dakina arobaini na saba mchana

Mariamu ametulizwa kutoka uchovu wake. Ametulizwa milele. Naomba msamaha Mariamu, kila mara tulipokosana na wewe. Pole sana…

Tarehe kumi na tisa Oktoba, saa tatu na dakika ishirini usiku

Ujirani wote wa sehemu ya Zahra hapa Gaza upo chini ya tishio. Minara yote ishirini na nne yanapigwa mabomu, mji yote kushahidiwa, mnara kwa mnara. Eh Mungu Eh Mungu!


Tarehe ishirini Oktoba, saa kumi na dakika hamsini na mbili jioni

Mbele ya Mungu, sisi tulio Gaza na mashahidi wa kifo au mashahidi wa ukombozi na sote tutangoja kujua tunaangukia wapi. Sote tunangoja Mungu, kiapo chako ni cha ukweli. 


Jioni ya tarehe ishirini Oktoba, Hiba Abu Nada alishahidiwa na familia yake baada ya kupigwa mabomu nyumbani kwao, ujirani wa Manara pale Khan Yunis.