Husam Maarouf

Mshairi aliyechapisha  “Death smells like glass”, “The barber loyal to his dead customers”  na riwaya  “Ram’s Chisel”.

Kabla ya vita, Husam aliandika mashairi kwa vipindi vifupi kwenye mtandao wa facebook.

Septemba 18, wiki tatu kabla ya mauaji ya kimbari, saa moja na dakika arobaini na nne usiku

Nywele zako zimefungwa begani mwako hiyo ni nathari. Nywele zako zimefungwa begani mwangu…Huu ni ushairi.


Oktoba 8, saa tano usiku 

Wakati wa vita vya Marekani-Vietnam, Wavietnam walipata nguvu zaidi kiasi kwamba uongozi wa jeshi Merikani ulipoteza udhibuti juu ya vikosi vyake na machafuko yakaenena kati ya wanajeshi. Wanajeshi Merikani waliasi uongozi wa jeshi, na wakawa wanadumia dawa za kulevya kwa wingi. Wakati huo, Mkuu wa jeshi, Creighton Abrams alitangaza: ’Nahitaji kurudisha jeshi hii nyumbani kuiokoa.”

Wakati huu, utatimizwa wakati mmoja wa viongozi wa serikali inayokalia na yeyote atakayesalia katika jeshi lao na watu wao, warudi kutawanyika walikotoka.



Oktoba 9, saa saba na dakika thelathini na nne mchana

Gaza inaangamizwa. Inaonekana sisi wote tunalengwa. Hatini hadithi baada yetu. Ambieni ulimwengu jinsi Gaza invayobadilisha eneo baada ya kila masaa mawili.



Oktoba 9, saa saba na dakika arobaini na moja mchana

Umeme umekatwa huku Gaza kwa siku kadhaa, na mtandao unakuja ukiondoka. Labda utakatwa hivi karibuni. Labda uwepo wa Gaza utakatiliwa kwa mbali, na wakati huo jukumu la kusimulia hadithi litakuwa mikononi mwako. Eleza historia kwamba Gaza ilishinda nchi yenye nguvu zaidi duniani, ikavuta wenyeji wake kama kondoo, na ikawahamisha kwa dakika chache.




Oktoba 9, saa saba na dakika arobaini na tisa mchana 

Sauti za mashambulio bila kusitisha. Hatujawahi kushuhudia boriti ya moto inayozingira nyumba. Ukaliaji ulikuwa ukiwaamrisha wakaazi wa maeneo pembeni kuondoka, na sasa wakaazi wa kati ya Gaza waondoke. Vita vinatutekeza hapa. Nina hakika kwamba tutatenganishwa nanyi na tutakuwa pekee yetu chini ya moto.



Oktoba 9, saa nane kasoro dakika mbili mchana

Ukaliaji uliamua kuzidisha mzingiro wa Gaza na kukata umeme, maji na chakula. Hii inamaanisha kwamba kama tutabaki hai na kunusurika kwenye makombora, tutakufa kwa sababu ya ubora duni wa maisha na ukosefu wa vifaa. Watoto watakufa kwa kukosa maziwa, wazee watakufa kwa kukosa chakula au dawa. Nchi, pamoja, ziliunga mikono na jeshi hili lililodhalilishwa siku juzi kurejesha mwonyesho wa nguvu kwa gharama ya raia. Iwe laana wanaosabahabisha maafa kwa wengine wanaowazingira.



Oktoba 9, saa nane na dakika kumi na moja mchana

Nawaandikia bila kujua kama nitawandikia tena. Majibu ya jeshi lililoshindwa na lililodhalilishwa sio kawaida. Amerika imewapa silaha zaidi kama kamwe kabla, na yote wanayofanya ni kubomoa nyumba juu ya vichwa vya wakazi, kuwalenga watoto na wanawake, na kuharibu misikiti. Nawaandikia kati ya vita tofauti na vya nyuma, na uwezekano wa kuishi wakati huu unaonekana kuwa nadra sana. Mashambulizi yanaongezeka kwenye nyumba. Watu hapa wanafifia kadamnasi na yanayoendelea. Hakuna mtu anayeweza kumpa mwingine usalama. Hata baba kwa mtoto wake mdogo hawezi kumpa usalama sababu yeye mwenyewe anaupoteza kwa wakati huu.



Oktoba 9, saa kumi na dakika nane alasiri

Kumbana na janga kwa kupaza sauti, kwa mkono wako, kwa kuandika, kwa chochote isipokuwa kimya. Historia haikumbuki kimya.



Oktoba 9, saa kumi na dakika ishirini na mbili alasiri

Baada ya shambulio la anagani, naskia sauti ya kioo kikivunjika ndani yangu. Nadhani ni tumaini!



Oktoba 9, saa tano kasoro dakika moja usiku

Ni kama tunapiga makofi kwa mkono mmoja!



Oktoba 9, saa tano na dakika kumi na mbili usiku

Uanadamu upo katika kiwango chake cha juu zaidi cha ustaarabu, kweli? Namshuhudia Mungu, huu ni uongo mkubwa. Ukoloni mbaya -mbaya zaidi katika historia- pamoja na ulimwengu uliostaarabika, unasimama na kushuhudia, unakubali kwamba umeanza kuzuia Gaza kutoka kwa maji, umeme na chakula. Ulimwengu uliolilevya, uliopokea malipo na faida, haujali.



Oktoba 10, saa sita na dakika ishirini na tatu usiku

Kuhamisha wenyeji walio salama kutoka nyumbani kwao ni jambo la kusikitisha. Jeshi zembe linaendelea na ukatili wake na kutuma notisi za kuhamisha kwenye vitalu vya makazi, vinavyo hifadhi mamia ya familia kwa ajili ya kushambuliwa.



Octoba 10, saa tano na dakika ishirini na mbili usiku

Kile Kinachotendeka Kaskazini mwa mji wa Gaza ni cha kutisha sana. Mungu alinde watu wa eneo la Karama na mazingira yao.




Oktoba 11, saa kumi na mbili asubuhi

Gaza haishughuliki na taswira au sifa zake, bali msingi wake uliochangaywa na majivu. Eneo hili la ardhi liliolimwa na maji ya bahari, lina ladha ya chumvi lakini ladha tamu, ladha kali ambayo inayaondoa uwezo wa kutamka. Gaza ina mtindo wake usioelezeka na usiowezeka kufutwa. Hii ndio inayofanya maadui zake wawe bila nguvu, wakimezwa na eneo lake ndogo kama paka inavyomeza hofu yake. Gaza ni mahali mbaya zaidi kupiga picha. Gaza ni sehemu maridadi zaidi ya kumbukumbu na hamu.Gaza kamwe haiji, inaelea katika machozi yake. Gaza kamwe hairopoki, lakini inadhihirisha kuishi kwa milipuko. Gaza iliyounganishwa na udongo wa Mungu na inayoendelea kubadilika, haina utulivu na hakuna maisha bila makafara.Yeyote anayeishi Gaza anafahamu kwamba, ni mahali kama mtoto ambaye anayehitaji kutunzwa, na anayeondoka Gaza anakuwa tasa.



Octoba 11, saa sita kasoro dakika tano usiku 

Nadhani ni lazima mufanye zaidi ya maombi na kuonyesha mshikamano. Tokeeni barabarani na mshinikize viongozi wenu waoga. Gaza, pamoja na kila mtu ndani yake itafutwa kwenye ramani kwa siku kadhaa.



Oktoba 12, saa sita na dakika nane mchana

Katika hospitali ya Al-Shifa Gaza, miili imepangwa  wazi kwa sababu vyumba vya kuhifadhi maiti haviwezi kumudi idadi kubwa ya mashahidi.



Oktoba 12, saa sita na dakika thelathini na nne mchana 

Ni jambo la kusikitisha, kujaribu kushawishi  ulimwengu kuwa mnakufa.



Oktoba 12, saa nane kasorobo mchana

Mabomu ya Gaza ni ya kudhuru. Ee Mungu Ee Mungu



Oktoba 13, saa moja kasoro dakika tisa jioni

Babu, niliurithi hadithi yako pia.

Nimekuwa mkimbizi kwa mara ya pili.



Oktoba 15, saa moja na dakika kumi na tatu  

Eh nalia nyumbani kwangu



Oktoba 19, saa tano asubuhi

Vita ambavyo havitamatishi kututekeza  ili ustaarabu uweze kuthibitisha utawala wake.

Vita vinavyozidi kuwa kizito.

Vinakanyaga siafu,vinawaangamiza, ili waweze kufanikisha njia ya udhalimu.

Ee dunia, sisi ni makoloni ya siafu,vikundi vidogo kwa watu wanaotapakaa nasibu.

Hatuwezi ishi wala kutoweka.

Kila tu tunachoweza ni kufungua midomo yetu kwa makombora.

Sisi ni watu duni wanaotokea kwenye unga wa bunduki.

Hatujui namna vile jua linachomoza, wala hatujui namna vile vita vinatua.

Tunabadilisha sauti yetu na mayowe, kuhakikisha kuwa hatujafa.

Sisi ni idadi iliyofifia, hatuhitaji kufutwa wala kudhibitishwa.

Komeni kuandika mgongoni mwetu:Hiki ni kifo kinachoibuka



Oktoba 22, saa kumi na mbili jioni 

Shusha pazia,

Funga Gaza kwenye sanda kubwa,

Endeleeni na maisha yenu ya bei rahisi

Endeleeni kimya na maisha yenu





Oktoba 25, saa saba na dakika ishirini na moja mchana

Hawajui kuwa maelezo yetu hapa yanamea kama mimea. Hawawezi elewa maana ya kijani kwenye ardhi hii.



Oktoba 27, saa kumi kasoro dakika tano alasiri

Sijui jinsi ya kuacha marafiki, 

siwezitamatisha muungano wangu kwa vitu.

Ardhi hii ni rafiki yangu ambaye siwezimwacha,

licha ya kiasi gani inaripuka usoni mwangu



Oktoba 29, saa tisa na nusu mchana

Maji yamekuwa nadra hapa, kwa sababu vituo vya kuondoa chumvi vimesimamishwa. Na mkate baada ya kulipua mikate, haupatikani tena kwa kila mtu, kiasi kwamba familia wanapanga foleni kupata Qurshalleh. Leo ni nilikutana na mtu ambaye aliapa kuwa kwa familia yake wamekuwa wakila biskiti kwa siku tatu kwa sababu hawawezi kupata mkate.


Oktoba 31, saa kumi na moja na robo jioni

Ee Bwana


Novemba 1, saa moja na dakika thelathini na sita jioni

Mungu wangu, huu ni huzuni? Na nilidthani kwa miaka mingi Nilijua tu!


Novemba 4, saa nne kasoro dakika saba, usiku

Mtoto amabaye alikuwa anafunzwa na mamaye kutembea, walipata ardhi ilinyakuliwa ghafla chini ya miguu yao.

Mtoto aliendelea kutembea, na hakusimama. 

Sikiza nami, mwendo wake 

Angalia meno yake machache…

Kombora bado haijawafikia.


Novemba 6, saa saba na dakika kumi na saba mchana 

Mbinu ya mazishi ya kisasa.

Hamna miili kamili, bali tu kundi la sehemu za miili zilizolala chini ya vifusi.



Novemba 6, saa tatu kasoro dakika moja usiku

Bwana, hakuna ardhi wazi ya kuzika wafu.

Je kama ungewafufua?


Novemba 8, saa nne kasoro dakika tatu asubuhi

Hapa, kwa kila muda mzuri tunaunda, kwa kila kicheko cha moyo, tunahisi hofu ya kinachokuja na hofu yetu daima imekuwa mahali pake.


Novemba 13, saa moja na dakika ishirini na nane jioni

Unawezaje kuwashusha watu kama meno halafu utarajie kicheko?



Novemba 17, saa nane na dakika nane mchana 

Mkono mmoja pekee unaweza kufikia na kuchukua nafasi ya taswira ya mwili dhaifu. 



Novemba 17, saa moja na dakika kumi na sita jioni

Nani hajazoea kukuskia, atafanya nini ukilipuka?



Novemba 27, saa saba na dakika thelathini na nne jioni

Mpaka tuwe nyumbani tena, hatuhisi kitu na hakuna cha dhamani. Maisha yetu yanabebwa,yakirushwa juu, na kwa kila wakati, tunahofia kuwa itapomoroka chini.



Husam alihamishwa kuenda Rafah, na anaendelea kuandika…